Pages

Pages

Wednesday, October 09, 2013

Unadhani hapa Rais Kikwete anamuagiza nini Dkt Abdallah Kigoda waziri wa Viwanda na Biashara na mbunge wa Handeni?

04Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (wa kwnza kulia) akiteta jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda (katikati) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi (wa kwanza kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kuzalisha dawa za kuulia viluwiluwi vya mbu wa malaria kilichopo nje kidogo ya mji wa Kibaha mkoani Pwani.

Kigoda ni Mbunge wa Handeni, huku akiwa mmoja wa mawaziri waliodumu kwa vipindi kadhaa kwa serikali ya Tanzania tangu utawala wa Rais Benjamin Mkapa na sasa mheshimiwa Kikwete, jambo linaloonyesha kuwa anaaminika na ana uwezo wa kuiletea maendeleo Tanzania. Je, unadhani hapa Rais Kikwete anamuagiza nini Kigoda katika tukio hilo kama picha inavyojieleza? Kama unajua tujulishe kwa email hii, kambimbwana@yahoo.com au +255712053949......

No comments:

Post a Comment