Pages

Pages

Saturday, October 19, 2013

Simba na Yanga wayeyusha pambano la ngumi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

PAMBANO la bondia Kalama Nyilawila na Sado Philemon, lililopangwa kufanyika katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Oktoba 20 mwaka huu limeahirishwa kutokana na kupisha mchezo wa Simba na Yanga.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa pambano hilo, Ibrahimu Kamwe, alisema kuwa pambano limeahirishwa kupisha mchezo huo wa watani wa jadi.


Sasa mabondia hao watapigana Novemba 3 mwaka huu katika ukumbi huo huo huku ukitanguliwa na mapambano mbalimbali ya vijana.


“Mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni pamoja na Mwaite Juma, Shedrack Ignas, Ajibu Salum, Martin Richard, Mbena Rajab, Godwin Mawe, Ibrahim class, Rashid Ali na Hassan Kiwale.


“Wengine ni Harman Richard, Kassim Chuma, Shaban Manjoly, Yona Miyeyusho, Julius Thomas,  Abdalla Ruwanje na Bakari Zoro,” alisema Kamwe.


Patashika hii imeandaliwa na Kamwe kwa kupitia Big Right Promotion yenye mikakati ya kuinua mchezo wa masumbwi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment