Pages

Pages

Sunday, October 13, 2013

Serikali ya Denmark yaahidi kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya afya na uchumi

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,Ummy Mwalimu  akiongoza maandamano ya wanawake walipokuwa wakiingia uwanja wa Mkwakwani kusherehekea maadhimisho ya siku ya msichana Duniani mbayo yalikwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wasichana wa mkoa wa Tanga unaoendeshwa na shirika la Tawode chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Denmark kupitia (DANIDA)

Burhani Yakub, Tanga
Tanga.Serikali ya Denmark imeahidi kuendelea kutoa msaada kwa maeneo mbalimbali nchini yatakayojikita  katika  kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto wa kike ili kuwawezesha kuinua hali zao za maisha kiuchumi
na kiafya.

Ahadi hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa balozi wa Denmark nchini, Ester Msuya wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wasichana wa Mkoa wa Tanga unaoendeshwa na shirika la Tanga Woman Development Initiative (Tawode)na kufadhiliwa na ubalozi huo kupitia DANIDA).

“Mkakati wa sasa wa Serikali ya Denmark kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa unaitwa “Haki ya maisha bora”tunajua kwamba uwekezaji ulio bora ambao Serikali yoyote inawaza kufanya ni ku-elimisha watoto wa kike”alisema Msuya.

Mwakilishi huyo wa balozi alisema Serikali ya Denmark inaamini katika haki za mtoto wa kike na mwanamke kupata elimu au angalau fursa ya kupewa stadi za maisha ili kuishi maisha bora na kuchangia katika maendeleo ya jamii kwa ujumla
Alilipongeza shirika la Tawode kwa kufanikisha mchakato wa kuanza kwa mradi huo wa kuwajengea uwezo wasichana wa mkoa wa Tanga na akaahidi kuwa ubalozi utatoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha mradi huo.

Akitoa melezo kabla ya kuzinduliwa mradi huo,Mwenyekiti wa Tawode ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Ummy Mwalimu alisema  lengo la kuendesha mradi huu ni kutokana na ukweli kwamba mtoto wa akike anabiliwa na changamoto nyingi kuliko wa kiume likiwamo suala la kutojitambua .

Alitolea mfano wa tafiti zilizopo za viashiria vya ukimwi na malaria nchini zilizofanyika mwaka 2011 na 2012 zinaonyesha kiwango cha maambukizi kwa wasichana ni cha juu kuliko wavulana hususani walio katika umri wa miaka 23 na 24.

Alisema maambukizi kwa wasichana walio katika umri kwa kati ya miaka 23 na 24 ni asilimia 6.6 wkati kwa wavulana wa umri kama huo ni asilimia 2.8 pekee.

Mradi huo ulizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye alipokea maandamano ya wanawake na  wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali mkoani hapa na pia alikagua mabanda ya maonyesho ya kazi za mikono zinazofanywa na wanawake.
                                      

No comments:

Post a Comment