Pages

Pages

Saturday, October 05, 2013

Maandamano ya kupinga ujangili wa tembo yalivyochafua jiji la Arusha jana

Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo hao.
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akionesha moja ya vibao ambavyo vinawaonesha Tembo wakati wa Matembezi hayo ya amani.
Kutoka kushoto ni Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki, Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert Chambulo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Magesa Mulongo.
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Matembezi ya Siku ya Tembo Duniani.
 Baadhi ya Wanaharakati wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani
Umati wa wananchi kutoka Arusha pamoja na wadau wengine kutoka Mikoa na nchi mbalimbali wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani yaliyo Fanyika Arusha Leo
 Hawa ni Watoto Shupavu kabisa waliojitolea Mstari wa mbele katika Matembezi ya Tembo leo
 Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisaini katika moja la bango la siku ya Tembo , ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
 Maandamano yakiwa yanaendelea
 Wa kwanza kutoka kushoto ni Mr. Peter ambaye ndiye alikuwa katika kamati kuu ya Maandalizi ya Siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, na pia Makamu mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours operators akiwa katika matembezi hayo
Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akiongoza maelfu ya watu wakiingia katika viwanja vya AICC ambapo ndipo ilikuwa kilele cha Matembezi hayo
 Afisa Mtendaji wa Chama cha Wakala wa Utalii TATO Ndugu Sirili Akko akitoa Maneno machache kabla ya ufunguzi Rasmi wa Kilele cha Matembezi ya Tembo Duniani.
 Meza kuu wakiongozwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki wa nne kutoka kushoto wakiwa wamesimama kwa mda wa dakika moja kuwakumbuka Waliokufa katika Tukio la Westgate Kenya pamoja na Tembo walio uwawa .
 Mc akiwa anaanza Tukio rasmi kwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali kwa ajili ya Kutoa salam zao na Risala
 Dr. Alfred kikoti Akitoa Mada yake juu ya Idadi ya Tembo ambao wamebakia , pia kuelezea kutokomeza kwa Biashara haramu ya uuzaji wa uuzaji wa Meno ya Tembo, na kusisitiza Tanzania inategemea Tembo katika Utalii.
Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Ndugu Wilbert Chambulo akielezea juu ya kusimamisha biashara kubwa ya Meno ya tembo ambayo inaongozwa na Nchi ya China na kuziomba Nchi zengine kusimamisha Biashara hiyo Haramu .
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya  Mongela wa Arusha Akimkaribisha Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Magesa Mulongo akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushiriki kikamilifu zoezi la matembezi ya siku ya Tembo Duniani na kumkaribisha Mgeni Rasmi Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki  kutoa hotuba yake.
Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na wanaharakati waliofika katika siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, kwa kutoa Salamu kutoka kwa Muheshimiwa Rais Kikwete kwamba Oparesheni ya kutokomeza majangili imeanza na Haitasimama.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akikabidhi vyeti kwa Shule Zilizo Shiriki Katika Matembezi ya Tembo Duniani
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kahasheki akipokea zawadi kutoka kwa TATO Anaye mkabidhi zawadi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa TATO Mr. Peter
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mlongo akipokea zawadi kutoka TATO Anayemkabidhi ni Bi. Tibaijuka
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Ndugu. Allan Kijazi akitoa neno la Shukurani wakati wa kufunga Kilele cha siku ya Matembezi ya Tembo Duniani leo
Hawa ni Wale waliotembea katika Matembezi ya Kupinga mauaji ya Tembo Kutoka Arusha hadi Dar es salaam Mwendo wa Kilometa 650 kwa Siku 12 Kutoka kushoto ni Binti Mdogo mwenye umri wa Miaka 20 Kaptorina Manange,Mkazeni Y. Mkazeni, Rehema Y. Najema, na Livingstone Y. Mkazeni.

Maandamano haya yalitokea Jirani na Cultural Heritage Hadi Viwanja vya AICC Kijenge Jijini Arusha, Matembezi yaliyo andaliwa na Tanzania Association Tours Operators (TATO)

No comments:

Post a Comment