Pages

Pages

Tuesday, October 22, 2013

Kivumbi cha Nkhwamba na Azam kurudiwa tena kesho

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MECHI ya kusisimua kati ya Nkhwamba na Azam zinazoshiriki Kombe la Kata ya Mrijo, iliyopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma, itanarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mrijo wilayani humo.


Mechi hiyo ni marudio baada ya ule uliochzewa Alhamis iliyopita kumalizika kwa daakika 90 huku zikifungana bao 1-1 hivyo kuamuriwa kuongezwa dakika nyingine 30, ambapo hata hivyo hazikuchezwa kutokana na giza kuingia, hivyo kuahirishwa hadi kesho Jumatano.


Akizungumza kwa njia ya simu akitokea wilayani Kondoa, moja ya wawezeshaji wa timu ya Azam yenye kushirikisha vijana wenye umri mdogo, Rashid Dogodogo, alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa na mvuto wa aina yake katika Kata hiyo wilayani Kondoa mkoani Dodoma.


Alisema mechi hiyo ni hatua ya robo fainali, huku mashindano hayo yakishirikisha timu mbalimbali zenye uwezo wa juu wa kucheza soka na kufurahisha wadau wengi wa mpira wa miguu wilayani humo.

“Mchezo huu utachezwa kwa dakika zote 90 baada ya juzi kushindwa kupatikana mshindi, hivyo ni matumaini yetu kuwa mchezo huu utakuwa wa aina yake na kufurahisha watu wengi.

“Mbali na mechi ya Azam na Nkhwamba itakayochezwa  Jumatano, pia Ijumaa iliyopita kulikuwa na mchezo wa kusisimua kati ya Kimetro na Kambugwe, huku Kambugwe ilikifanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Nkhwamba,” alisema.


Timu ya Azam inafadhiliwa na Khadija Rashid, Khamis Msakati na Dogodogo, wakati wafadhili wa Kimetro ni Hassan Choma na Omari Kipara, huku kocha wa Nkhwamba akiwa ni Shaban Juma Baba, wakati ile ya Azam inanolewa na Hamza Ramadhan na kocha wa Kimetro ni Kaifa Nduko.


Baadhi ya timu nyingine zinazoshiriki mashindano hayo ni Ndido, Njolo, Wakata Miwa, Mapango na nyinginezo zinazoshiriki patashika hiyo ya Kombe la Kata ya Mrijo, wilayani Kondoa mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment