Pages

Pages

Tuesday, September 17, 2013

Umuhimu wa kutambua na kuthamini kabila na asili ya watu wenye kabila la Wazigua, wilayani Handeni, mkoani Tanga



Na Handeni Kwetu, Blog
NAAM! Wazigula au wazigua kama wanavyojulikana ni watu wa kabila moja kutoka eneo la karibu Bahari Hindi na baina ya Dar es Salaam na Tanga, nchini Tanzania. 
Watu wenye asili ya Handeni, ambao wengi wao ni Wazigua wana vykula vya kila aina. Mwishoni mwa mwaka jana dada huyu aliyetambulika kama Rehema Mbwana, alikutwa kijijini Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, akionja mboga aina ya hombo.

Mwaka 1993 idadi ya Wazigula ilikadiriwa kuwa 355,000 na Lugha yao wanayotumia ni Kizigula, kama kinavyojulikana kwa watu wengi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za hapa na pale, kuna mengi yalitokea kipindi cha nyuma cha kuwapo wilaya ya Handeni, ambayo baadaye iligawanyika na kuzaliwa wilaya ya Kilindi, inayoongozwa na DC Suleiman Liwowa. Wilaya ya Handeni kwa sasa ipo chini ya DC Muhingo Rweyemamu.

Mwaka 1961, 62 na kuendelea, wilaya ya Handeni, kwa wanaoijua hadi leo kuna mlima unajulikana kama Kwambwembwele. Enzi hizo, kuna mzee mmoja aliishi juu ya mlima huo akijulikana kama Mhandeni. Huyu mzee alikuwa akivuta Ndoyo. Ndoyo kwa kizigua maana yake ni Kiko.

Basi, watoto waliokuwa enzi hizo, yani mwaka 1961 na kuendelea walikuwa wakiona moshi ukitoka na kuambiwa namna mzee huyo alivyokuwa akivuta sigara hiyo. Kwa wanaojua namna wazee hawa walivyokuwa wakivuta sigara zao, tumbaku watakubaliana na mimi kuwa sigara zao zilikuwa kubwa na zilishindwa kuzimika haraka.

Kuna wazee waliokuwa wakiwasha sigara zao kijijini kwao na kutembelea umbali unaochukua saa sita au saba na bado tumbaku lao halijazimika. Aidha, kwenye mtandao wa wikipedia kunaonyesha pia kumbukumbu nyingi juu ya kabila la Wazigua.

Mengi yaliyoorodheshwa humo yana ukweli na watu wa Handeni na 
wasiokuwa Handeni wanaweza kuitumia katika kutafiti baadhi ya mambo muhimu kwa ajili ya kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Wazigua ni mojawapo wa makabila ya asili ya mkoa wa Tanga. Wazigua ambao lugha yao ni ya jamii ya lugha za kibantu yasemekana walikuwapo mkoani Tanga, wilaya ya Handeni kwa karne nyingi zilizopita hadi leo hii wameongezeka mara dufu kutokana na vizazi vyao kuzaliana siku hadi siku, mijini na vijijini kwa ujumla.

Wazee wa zamani walichambua maana ya neno Zigua kuwa ni kuchukua au ukamata eneo na miaka hiyo yote Wazigua walipigana vita na kuyashinda makabila ya Wabondei na Wasambaa.

Makabila hayo yaliyoshindwa vita yalikimbiliia maeneo ya mabondeni na mengine kusambaa milimani, Wabondei huko Mabondeni, na Wasambaa walisambalia milima ya usambara.

Na ndio chanzo cha majina ya makabila haya, kwani kabla ya hapo walikuwa wakiishi pamoja kama koo za jamii moja. Na walijulikana kwa jina la Boshazi maana yake Bondei, Zigua, Sambaa.

Maelezo haya ni majibu ya msomaji wetu aliyeuliza katika group forum ya Handeni Kwetu iliyokuwa katika mtandao wa kijamii facebook akitaka kufahamu asili ya Wazigua na yametokana kwenye vyanzo mbalimbali, ukiwamo mtandao wa wikipedia.

Kama una maoni au ushauri, tafadhali tuandikie, mbwanakambi@gmail.com, babamkubwa@yahoo.com au +255712053949

No comments:

Post a Comment