Pages

Pages

Wednesday, September 04, 2013

Mtunisha misuri awa kivutio uzinduzi wa Simtank mpya


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MTUNISHA misuri anayefanya vizuri katika sekta hiyo nchini, Mussa Mohamed maarufu kama 50 Cent, alikuwa kivutio katika uzinduzi wa Simtank mpya, yanayozalishwa na Kampuni ya SILA AFRICA.
Mtunisha misuri anayejulikana kwa jina la Mussa Mohamed, akipamba uzinduzi wa SimTank jana, jijini Dar es Salaam.Kulia na kushoto kwake ni mabinti waliokuwa wakishiriki nao kwenye hafla hiyo ya aina yake.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mtunisha misuri huyo ambaye pia alishiriki katika mashindano mbalimbali likiwamo la Dume Condom, alisema kuwa ni fahari yake kuwa kwenye uzinduzi huo.

Alisema kuwa sekta yao hiyo ya kutunisha misuri imekuwa kwenye nafasi nzuri kwasababu ya kutumiwa na makampuni makubwa.

“Nashukuru kuwa kwenye historia ya uzinduzi wa matenki mazuri ambayo hata kama yakianguka hayawezi kupasuka kirahisi,” alisema.

Aidha katika uzinduzi huo ambao walimuita mtunisha misuri huyo kuburudisha, Meneja Mkuu wa SILA AFRICA, Alpesh Patel, aliusifia uzalishaji huyo kwa madai kuwa ni sehemu nzuri kwa Watanzania wote.

Tangu asubuhi kuanza kwa shughuli huyo, mtunisha misuri huyo ndiye aliyekuwa kivutio kikubwa kwa wageni waalikwa kutokana na kuonyesha mwili wake na jinsi alivyoweza kuuandaa kimazoezi.

No comments:

Post a Comment