Pages

Pages

Wednesday, September 04, 2013

JB awapa somo wasanii wa Tanzania


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NYOTA wa filamu hapa nchini, Jacob Stephen (JB), amesema ili sanaa ipige hatua ikiwamo ya uigizaji na uimbaji, inahitaji mipango ya uhakika pamoja na kujituma kwa wasanii wote kwenye kazi zao.
Msanii wa filamu Tanzania, Jacob Steephen JB.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, JB alisema kuwa wasanii wasiotambua hilo, hawawezi kusonga mbele na kuendeleza soko lao.

Alisema ingawa muziki hasa wa kizazi kipya na filamu unachanja mbuga, ila wanapaswa kuongeza bidii kwa ajili ya kuwa juu zaidi.

“Huu ni wakati wa kila msanii kuweka mkazo katika ufanyaji wake wa kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo yake katika sekta ya sanaa kwa ujumla.

“Naamini wote tukifanya hivyo tutazidi kuwa juu na kufanikisha maendeleo yetu pamoja na Taifa kwa ujumla, ukizingatia kuwa sanaa ni kazi,” alisema.

JB ni miongoni mwa wasanii wa filamu wenye mipango kabambe na wanaokubalika kwa kiasi kikubwa kutokana na utendaji wake wa kazi.

Baadhi ya Filamu lizochezwa na JB ni pamoja na Regina, DJ Benny na nyinginezo zilizomuweka juu katika tasnia ya filamu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment