Pages

Pages

Sunday, September 08, 2013

Makubwa ya vita ya dawa za kulevya baada ya meli kukamatwa Italia ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya

cegrab-20130907-235714-313-1-522x293
Meli iitwayo Gold Star ambayo ilikuwa inafatiliwa kwa siku kadhaa, imekamatwa karibu na pwani ya Italy ikiwa na zaidi ya tani 30 za dawa za kulevya ambapo Polisi wa Italy wamesema documents zinaonyesha ilisajiliwa Tanzania.

Taarifa nyingine ya polisi imesema kabla ya kusafiri kutoka Turkey ilipewa ruhusa kutoka Tanzania na thamani ya mzigo huo ni pound millioni 50 ambayo kwa pesa za kitanzania ni kama 126,582,278,481.

Kwenye sentensi ya tatu, taarifa imesema Meli ilikuwa na crew ya watu kutoka nchi za Egypt na Syria ambapo mzigo wote wameupakia kutoka Uturuki.

Unaambiwa baada ya kuona mchezo wao umefahamika, watu waliokuwemo kwenye meli waliamua kuanza kuichoma moto meli hiyo ambapo pia kati yao, watu tisa walijirusha baharini kwa nia ya kutaka kukimbia lakini wakakamatwa na kukutwa hizo dawa za kulevya aina ya hashish ambazo thamani yake inagonga kwenye £50m.


Credit: Millard Ayo

No comments:

Post a Comment