Pages

Pages

Friday, September 20, 2013

Kaseba ataka wadau waanzishe kambi za masumbwi



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema kuna haja ya wadau wa ngumi na mabondia nchini kuanzisha kambi za kulea na kufundisha ngumi vijana mbalimbali wanaopenda mchezo huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Kaseba alisema hali hiyo ikiendelezwa itachangia kuleta hamasa zaidi katika masuala ya masumbwi.

Alisema kuwa nchi mbalimbali wamekuwa wakifanya mtindo huo kwasababu unachangia kwa kiasi kikubwa kuleta ushindani kwa mabondia.

“Mimi nina eneo langu ambalo mabondia kadhaa hupatikana au kuja kujinoa mara kadhaa, hivyo kuna kila sababu wadau wengine kufanya mchakato huo.

“Tukifanya hivyo tutaweza kuinua kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mchezo wa masumbwi hapa nchini, hivyo huu ni wakati wa kuingia katika mipango yenye kujenga,” alisema.

Kaseba anaheshimika katika ramani ya masumbwi, huku akiendeleza mabondia kadhaa, akiwapo mwanadada Pendo Njau, anayekubaliwa na wengi kutokana na ubora wake.

No comments:

Post a Comment