Pages

Pages

Friday, September 20, 2013

CANACO:Tukianza uchimbaji wa madini wilayani Handeni tutafanikisha ajira za kutosha kwa wananchi



Na Mwandishi Wetu, Handeni
MENEJA Utafiti wa Kampuni ya CANACO inayojishughulisha na mambo ya madini wilayani Handeni, mkoani Tanga, Bavon Mwaluko, amesema kwamba wanakusudia kuleta ajira kwa wananchi na wakazi wa eneo lote la Magambazi, mara baada ya serikali kuruhusu kuendelea na shughuli hiyo.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Serikali ilizuia kwa muda shughuli za uchimbaji na utafiti wa madini katika eneo hilo mapema mwaka huu kwa ajili ya kuangalia kwa kina mchakato mzima wa kazi hizo.

Akizungumza hivi karibuni wilayani Handeni, Mwaluko alisema shughuli za uchimbaji wa madini zinahitaji nguvu kazi, hivyo endapo wataanza kazi hiyo wanananchi watanufaika.

“Tuliingia katika eneo la Magambazi mwaka 2007 kwa ajili ya kuendesha shughuli za utafiti wa madini yaliyoko kama hatua za awali kabla ya kuanza kazi ya ujenzi wa mashine kwa ajili ya uchimbaji.

“Tulikubaliana na wenyeji waliokuwa wakimiliki maeneo hayo ambao walikuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji mdogo na tulitumia fedha nyingi kuwalipa fidia hivyo kwa sasa tunachosubiri ni ruhusa ya serikali ili tuanze kazi ya uchimbaji na hakika tutaweza kuajiri watu wengi katika kuendeleza mradi huo,” alisema Mwaluko.

Kwa mujibu wa Mwaluko, kabla ya kuanza zoezi la uchimbaj ni lazima kufanya tafiti ili kujua tabia za miamba ukizingatia mingine inaweza kuwa na milipuko au ni sehemu ya chanzo cha maji na kuchangia uharibifu wa mazingira.

No comments:

Post a Comment