Pages

Pages

Sunday, August 25, 2013

Yanga haina mpinzani, ndiyo iliyoshinda kwa mabao mengi katika mechi za kwanza za ufunguzi wa patashika hiyo



Kivumbi cha msimu mpya wa ligi ya Tanzania Bara, ambapo pichani ni beki wa Ashanti United, Ramadhani Malima akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Hussein Javu, katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana, katika mechi iliyomalizika kwa Yanga ikushinda bao 5-1.
 
KWA kushinda kwa bao nyingi mno katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Tanzania Bara, timu ya Yanga sasa inaongoza ligi hiyo kwa kufanikiwa kuwachachafya kwa mabao 5-1 dhidi ya Ashanti United ya jijini Dar es Salaam, huku ikifuatiwa na timu ya Coastal Union ya Wagosi wa Kaya kwa kuwafunda mabao 2 kwa 0 timu ya JKT Oljoro ya jijini Arusha.

Mechi nyingine zilizochezwa jana, timu ya Mgambo Shooting ya wilayani Handeni mkoani Tanga ilishindwa kutumia uwanja wake wa Mkwakwani baada ya kufungwa bao 2-0 na JKT Ruvu ya mkoani Pwani, wakati timu ya Simba SC, walianza kwa sare ya bao 2-2 dhidi ya Rhino Rangers ya mkoani Tabora.

Timu ya Mbeya City nayo ilianza kwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar, huku Mtibwa Sugar ya Turiani mjini Morogoro nayo ikifungana bao 1-1 dhidi ya timu ya Azam FC, washindi wa pili wa ligi iliyomalizika.

Yanga imeonyesha kuanza vyema msimu mpya wa ligi hiyo, huku ikijigamba kuwa kikosi chao ni hatari na hakina cha kupoteza kwenye msimu mpya ulioanza jana Agosti 24.

 

No comments:

Post a Comment