Pages

Pages

Sunday, August 25, 2013

Mdogo wake Kanumba atangaza kutafuta mdosi ili apakuwe filamu yake



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII mchanga, Lameck Charles Kanumba, mdogo wake msanii nyota wa filamu hapa nchini, marehemu Steven Kanumba, amesema kwamba anatafuta kampuni ya kufanya nayo kazi ili aweze kufikia malengo.
Hiyo ni kutokana na kubanwa na bajeti katika kuandaa filamu yake ‘Charles’, licha ya kuiandaa kwa kiwango cha kutisha na dhamira ya kuteka soko hilo sanjari na kulinda jina la kaka yake.

Yoyote anayependa kuwasiliana na Lameck, ametoa namba zake hizi, +255 656865755, ambapo kwa sasa anaishi Sinza Uzuri, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, kijana huyo aliyekuja jijini mapema mwaka huu katika kumbukumbu ya marehemu kaka yake, alisema kuwa ili filamu iwe na kiwango kizuri inahitaji bajeti.

“Naomba kukutana na yoyote anayeipenda sanaa ya maigizo na filamu ili niweze kufanya naye kazi ya kutoa filamu zangu, huku nikiamini kuwa zitakuwa moto wa kuotea mbali.

“Hii ni kazi ambayo naiweza vizuri kutokana na kuwa na kipaji change, japo nasikitika kukosa mtu wa kuniongoza kutokana na matatizo ya Kidunia, yakiwapo kumkosa marehemu Kanumba,” alisema.

Lameck na marehemu Kanumba wamechangia baba, ambaye hata hivyo amekuwa akishindwa kuwalea, jambo linalowasababishia msoto katika kipindi cha maisha yao.

Kanumba ilimlazimu aje jijini Dar es Salaam kutafuta maisha ya sanaa, ambapo baadaye alifanikiwa na kuwa na jina kubwa kiasi cha sasa kuleta mkanganyiko kutokana na baba yake huyo kuzitolea macho mali zake.

Yoyote anayependa kuwasiliana na Lameck, ametoa namba zake hizi, +255 656865755, ambapo kwa sasa anaishi Sinza Uzuri, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment