Pages

Pages

Wednesday, August 21, 2013

Wazee wa Ngwasuma wajiziba mdomo wa majigambo



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, imesema kuwa imeamua kuelimika na kuziba midomo ya majigambo, kwasababu si njia za kuwaweka kileleni.

Ngwasuma inayoongozwa na Rais wa Vijana, Nyosh El Sadaat, imeyasema hayo jana kwa kupitia Mkurugenzi wake wa Fedha na Utawala, Kelvin Mkinga, ikisema kuwa majigambo hayawezi kuwaletea heshima katika muziki wa dansi.

Mkinga alisema kwa miaka kadhaa sasa, bendi ya FM Academia imezidi kufanya vizuri bila kuzalisha malumbano ya mara kwa mara na wanamuziki wao, pamoja na kufunga mdomo wao.

Alisema kuna bendi zinazojiendesha kwa majigambo, lakini jukwaani wanakuwa wepesi, hivyo kuwa njia za kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima mbele ya jamii.

“Tunashukuru kwasababu sisi tunataka kazi na sio majigambo ya mara kwa mara hasa katika vichwa vya habari, ukizingatia kuwa mpango huo hauna mbolea katika tasnia ya muziki wa dansi.

“Tunatunga nyimbo nzuri pamoja na kufanya shoo za aina yake ambazo ndio sababu ya kuiweka kileleni bendi yetu, hivyo hatuwezi kuacha msingi wa kazi zetu,” alisema.

Wazee wa Ngwasuma kwa sasa inatamba na wimbo wake wa Otilia, ulioimbwa kwa hisia za aina yake kutoka kwa waimbaji wake, akiwamo Patchou Mwamba, Pablo Masai na wengineo.

No comments:

Post a Comment