Pages

Pages

Sunday, August 04, 2013

Wakandarasi wilayani Handeni na Tanzania kwa ujumla, waaswa wasigeuza Halmashauri kuwa shamba la bibi



NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, amewataka wazabuni kujenga miradi ya maendeleo mkatika Halmasahauri nchini kwa kufuata masharti na weledi wao badala ya kuzigeuza Halmashauri hizo kama shamba la bibi kwa kuchota fedha na kutekeleza miradi chini ya kiwango.


Naibu Aggrey Mwanri, pichani.
Hayo yamesemwa na Mwanri baada ya kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa wodi ya kina mama wajawazito katika kituo cha afya cha Mkata inayosimamiwa na Kampuni ya Elcat Builders (T) Ltd hapo jana, katika ziara yake wilayani Handeni mkoani Tanga.

Alisema ni kawaida kwa wa kandarasi wanaopewa zabuni za usimamizi wa miradi kutotekeleza kwa kiwango kinachostahiki huku wakipoteza raslimali fedha ya serikali ambayo bila ya kuionea huruma nchi yao.

“Nakerwa nakitendo cha wakandarasi kuzifanya Halmashauri kama shamba la bibi la kuchuma fedha na kutekeleza miradi ya madudu, Mwenyekiti wa Halmashauri liangalieni hili na ikibidi muingile kati ili kuhakikisha mnazisimamia kwa ukaribu fedha za miradi zinazotolewa naserikali,”alisema Naibu Waziri

Naibu Waziri alionyesha kukerwa zaidi baada ya kusomewa taarifa na mkandarasi wa Wilaya kuwa mradi huo nia hadi ya Rais Kikwete aliyoitoa wa kati wa kampeni za urais nakuahidi kutoa fedha kiasi cha Sh 100 kwa ajili ya utekelezaji ahadi ambayo aliikamilisha.

Injinia Richard Mocha alisema kutoka namkandarasi huyo kuchelewesha ujenzi wa mradi huo ndipo walipo muandikia barua ya kusudia la kusitisha mkataba kutokana kupitisha muda wakukabidhi mradi huku jingo likiwa katika hatua za kupauwa.

“Mheshimiwa Naibu Waziri ujenzi wa mradi huu mpaka utakapokamilika utagharimu kiasi cha Sh Mil 96 huku kiasi kilichotolewa na Rais Jakaya Kikwete kiki wa nish Mil 100 na mpaka hatua iliyofikiwa ya ujenzi ni sh Mil 10 huku ujenzi ukiwa bado unaendelea.

Hata hivyo Naibu waziri alisema siku mia moja ilizopewa kampuni yao ya kuvunja mkataba alishauri zitakapokwisha mradi huo apewe mkandarasi mwingine ilijengo hilo likamilike kwa wakati na wananchi waweze kupatiwa huduma kwa haraka.

No comments:

Post a Comment