Pages

Pages

Sunday, August 04, 2013

Hamis Kiiza sasa amaliza filamu yake ya leo kesho ndani ya Yanga



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umefurahia kuwasili kwa mshambuliaji wao Kimataifa, Hamis Kiiza, akitokea nchini kwao Uganda, huku wakiingia naye mkataba wa miaka mwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.
Hamis Kiiza, pichani
Kiiza aliwasili juzi jioni akitokea nyumbani kwao Uganda, huku ujio wake ukitarajiwa kuwa ndio mwisho wa vuta nikuvute na kuwatia wasiwasi mashabiki na wadau wa timu ya Yanga.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa Kiiza amewasili na kujiunga na wenzake katika mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali, ikiwa ni baada ya kuingia naye mkataba wa miaka miwili.

Alisema kuwa tayari wameshaingia naye mkataba wa miaka miwili, huku wakiamini kuwa nyota huyo ataendelea kuitumia timu yao kwa nguvu zote.
“Kiiza amewasili nchini na kuingia naye mkataba wa miaka miwili, ambapo tunaamini kuwa tumekata ngebe ya waliokuwa wakidhani hatutaweza kumsajili tena nyota huyu wa Kimataifa.

“Kwa sasa limebaki jukumu lake na benchi la ufundi kwa ajili ya kumuandaa mchezaji huyu kwa ajili ya kuitumikia timu yetu ya Yanga,” alisema Kizuguto.

Kiiza alishindwa kuafikiana na Yanga mara kadhaa, ambapo hata hivyo Yanga kwa kupitia msemaji wao walishindwa kuweka wazi kiasi cha pesa walichokubaliana dhidi ya mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment