Pages

Pages

Saturday, August 10, 2013

Tindikali waliyomwagiwa mabinti wawili wa Uingereza, yaichafua Tanzania nje ya mipaka yake



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Taarifa za kumwagiwa Tindikali kwa raia wawili wa Uingereza waliokuwa wakifanya kazi ya kujitolea Visiwani Zanzibar, nchini Tanzania vimezidi kugonga vichwa vya habari ndani na nje ya nchi.
Tindikali inavyoshambulia mwili wa binadamu
Kirstie Trup na rafiki yake Katie Gee walikutana na dhahma hiyo, wakiwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yani Zanzibar, ambapo sasa wamerudishwa nyumbani kwao kwa matibabu.
Mhariri wa masuala ya Utalii wa Gazeti la Mirror, nchini Uingereza, aliandika hivi, “ninaweza kusema kwamba hakuna sababu ya kutokwenda Zanzibar kwa vile ni mahali salama, panafurahisha na kuna fukwe nzuri na mambo ya kihistoria yenye umaarufu mkubwa,” aliandika Nigel Thompson kwenye gazeti hilo.
Hizi ni miongoni mwa kauli mbalimbali zilizotolewa na wadau wa amani, utalii duniani, ikiwa ni saa chache baada ya raia wa Uingereza kumwagiwa tindakali, wakiwa Visiwani Zanzibar, Agosti 8 mwaka huu.

Kwa siku tatu sasa, magazeti mengi ya nchini Uingereza pamoja na televisheni zao zimekuwa zikiripoti habari hizo zinazozidi kuichafua serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mabinti hao wamefikishwa nyumbani kwao kwa ajili ya kupata matibabu, ikiwa ni baada ya kupata balaa hilo, ambalo watu mbalimbali wamekuwa wakiponda juu ya waliofanya unyama huo.

Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Ismail Jussa, ambaye pia ni kiongozi kutoka Chama Cha Wananchi (CUF), aliwajia juu waliotenda tukio hilo kwa madai kuwa wana lengo la kuichafua Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

"Hatuwezi kukaa kuchekea tukio hili maana linaweza kuiweka Zanzibar katika mtego mkubwa kwenye masuala ya Uchumi kwa kupitia sekta ya Utalii visiwani Zanzibar,” alisema.

Katika hilo, baadhi ya watu wamehusisha na Uamsho, ingawa uchunguzi bado haujawekwa wazi juu ya chanzo cha tukio hilo.

No comments:

Post a Comment