Pages

Pages

Monday, August 05, 2013

SIWEZI KUVUMILIA:Karibu Ligi Kuu, tuangalie ‘madudu’ yetu

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
LIGI yetu ya Tanzania Bara inavyopambwa, hasa katika maandalizi yake, utasema ni nzuri na yenye mvuto mkubwa hapa nchini. Utaona tambo za kila aina.
Leodgar Tenga, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Utaona jinsi wachezaji waliosajiliwa kwa ligi hiyo wanavyopambwa katika vyombo vya habari wakiona wao ndio kila kitu katika soka la Tanzania.

Lakini si ukweli huo. Katika miaka nenda rudi, Tanzania tumekuwa soka la kawaida kabisa, japo si sawa na wenzetu wa Tanzania Visiwani, yani Zanzibar.
Sisi soka letu zaidi lipo katika kurasa za magazeti. Ndio maana siku zote tunazalisha wachezaji wa kawaida na wasiokuwa na lolote katika soka la Tanzania.

Tuna wachezaji wenye majina makubwa akiwamo Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Kelvin Yondan, Juma Kaseja, Haruna Moshi ‘Boban’ na wengineo ambao miguu yao haijaweza kulifanya soka letu lipige hatua.

Japo mapungufu ya wachezaji wetu wa Tanzania mara kadhaa yanasababishwa na mfumo wa soka letu, kutoka katika vichwa vya viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), ila kujitambua nako kwa vijana hawa kunahitajika.

Hapo ndipo ninaposhindwa kuvumilia. Ligi ya Tanzania Bara inaanza Agosti 24 mwaka huu kwa viwanja kadhaa kuwaka moto kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo kuingia uwanjani.

Timu hizo zinawania taji la Vodacom linaloshikiliwa na Yanga iliyotwaa mwaka msimu uliomalizika ambapo tulishuhudia bingwa mtetezi Simba, akiangukia pua, huku akikosa hata nafasi ya pili.

Bingwa alikuwa ni Yanga ambayo pia imepata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa, Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam iliyoshika nafasi ya pili ikikata tiketi ya kucheza mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Pamoja na kunyakua nafasi hiyo kwa Yanga au Simba iliyoshindwa kulitetea, ila bado ligi yetu hatuoni ladha halisi na ushindani unaoweza kunyanyua soka letu.

Mara kadhaa ligi huwa tamu zaidi zinapokutana timu za kawaidam, yani Coastal Union ya mjini Tanga, Ruvu Shooting, ila si kwa mechi ya Simba na Yanga.

Zaidi utamu zaidi hukolea pale Yanga au Simba inapokutana na Azam au Coastal Union, ingawa wakati mwingine nguvu ya umma, yani ushabiki huleta mkanganyiko.

Siwezi Kuvumilia hata kidogo. Hivyo kuna kila sababu ya timu zetu za Tanzania kucheza soka la uhakika ili ligi yao iwe na nguvu kwa muda wote.

Tunataka mashabiki wao wafurahie burudani ya soka, ukizingatia kuwa wanalipa viingilio vyao halali kwa ajili ya kuunga mkono sekta ya mpira wa miguu Tanzania.

Timu ya Yanga ambayo ndio bingwa mtetezi, lazima ijuwe kuwa inaingia uwanjani kucheza soka la uhakika na sio kutumia mtaji wa wadau wao kuvuruga utaratibu.

Ni mara kadhaa sasa timu za Tanzania, hasa Simba na Yanga zinapoingizwa kwenye timu zinazopenda kutumia mtaji wao wanachama kununua mechi.

Na ndio timu hizo pia zinatajwa kuhujumu usajili wa wachezaji mara kwa mara. Simba ina uwezo wa kusajili mchezaji yoyote hapa Tanzania, ila baadaye inashindwa kuwatumia na kutumbukia katika shimo la upangaji wa matokeo.

Hii si njia nzuri ya kukuza na kuendeleza soka letu, hivyo lazima tuwe makini kama tunahitaji kuwa makini. Mpira ni ajira inayowapa utajiri watu wengi.

Dakika 90 tu za mchezo kati ya Yanga na Simba zinaingiza mamilioni ya shilingi. Usajili mmoja tu kwa Dunia ya leo, unamfanya nyota husika achote fedha lukuki.

Ukiacha wachezaji wa Tanzania wanaosajiliwa kwa fedha za kununua soda, ingawa baadaye hudaiwa wamevuna fedha nyingi, wenzao nje wanatembelea kwenye utajiri wa aina yake.

Hii ni kwasababu wameweza kuwa makini, huku wakitumia muda wao mwingi kufanya juhudi zao binafsi. Tanzania inaweza kufikia hatua hiyo, ila kwa kuendelea kujenga msingi imara wa soka letu, hasa kwa kuifanya ligi iwe na nguvu.

Timu zishinde kihalali na sio kununua mechi au wachezaji kucheza chini ya kiwango kwasababu mbalimbali, yakiwmao mapenzi ya timu wanazokutana nazo au kupewa ahadi ya chochote kutoka kwa wanazi wa Simba na Yanga.

Tukifanya hivyo, ligi yetu itakuwa na nguvu nje na ndani ya uwanja, hivyo kuwa mtaji pekee unaoweza kuongeza thamaani ya wachezaji wa Tanzania na kuwa thamani yao ya  kuonekana duniani kama wanavyotamba wengine.

Tukutane tena wiki ijayo.
0712 053949

No comments:

Post a Comment