Pages

Pages

Sunday, August 04, 2013

January Makamba, Kagasheki waipiga tafu Habari Group kusaidia watoto yatima jijini Dar es Salaam



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WANACHAMA wa Kikundi cha Waandishi wa habari wanaojihusisha na ujasiriamali (Habari Group), wametoa msaada wa vyakula na nguo wenye thamani ya sh. milioni moja kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima kwa ajili ya sikukuu ya Idd El Fitri.
January Makamba, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia
Msaada huo uliofadhiliwa na wadau mbalimbali ulikabidhiwa juzi, na wanakikundi hao ikiwa ni njia ya kuonyesha ushiriki wao katika masuala ya jamii.

Vituo vilivyokabidhiwa msaada huo ni Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Tahfidhil-Qur-An Al-Hidaya kilichopo Buguruni na kituo cha Al Furqaan Islamic kilichopo Chanika.

Mweka hazina wa Habari Group, Hellen Mlacky alisema kuwa msaada huo umechangiwa na wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Mwenyekiti wa Aisha Sururu Foundation, Aisha Sururu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mashekh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania,Sheikh Hamis Mattaka.

Wengine ni mmiliki wa wa maduka ya Silva Boutique Madam Nora na Mkurugenzi wa kampuni ya Quality Printers and stationaries,Amani sokko.

Alitaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na nguo, sukari, mchele, maharage pamoja na  mafuta ya kupikia.

“Sisi kama wanahabari wajasiriamali kikundi chetu ni cha kusaidiana na hivyo tumeona ni  vyemka na sisi tukashiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili nao washerehekee sikukuu kama watoto wengine wanaoishi na familia na jamaa zao,” alisema.

Akishukuru kwa msaada huo, Katibu wa kituo cha Tahfidhil-Qur-An Al-Hidaya, Abubakar Simba aliiomba jamii kuendelea kukisaidia kituo hicho ili watoto wanaolelewa waweze kupatiwa mahitaji yote muhimu.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Al Furqaan Islamic, Hamis Omari alishukuru kwa msaada huo na kuitaka jamii kuwaona watoto hao ni sehemu yao na kuwasaidia ili nao waweze kufanikiwa katika maisha yao.

No comments:

Post a Comment