Pages

Pages

Saturday, August 10, 2013

Simba watangaza uhondo wa tamasha lao kesho



SNURA, TUNDA MAN NA JUMA NATURE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Nature, Tunda na Snura kunogesha Simba Day
Ndugu Wanahabari,
Eid Mubarak

KESHO, Jumamosi tarehe 10 Agosti mwaka 2013, klabu ya soka ya Simba itaadhimisha kile kinachoitwa Siku ya Simba (SIMBA DAY) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu kwa lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi walizonazo.

Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.
Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo. Kutakuwapo pia na burudani ya muziki kutoka vikundi mbalimbali hapa nchini.

Kabla ya mechi ya Villa, kikosi cha pili cha Simba kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za vijana za timu za majeshi ya Tanzania kuanzia saa nane mchana. Mechi ya Villa inatarajiwa kuanza saa kumi na nusu nusu jioni.

Milango itafunguliwa kuanzia saa sita mchana na tiketi zitauzwa hapo hapo Uwanja wa Taifa. Viingilio vitakuwa ni Sh 20,000 kwa VIP A, 15,000 kwa VIP B, Sh 10,000 kwa VIP C, Sh, 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa na bluu na Jukwaa la Kijani itakuwa ni Sh 5,000.

Wachezaji nyota wa Simba msimu uliopita pia watatajwa na kupewa tuzo zao. Nyote mnakaribishwa.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

No comments:

Post a Comment