Pages

Pages

Sunday, August 11, 2013

Semina ya makamishina wa Ligi Kuu ya Vodacom kuanza kesho Agosti 12

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SEMINA kwa ajili ya makamishina wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa  waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza.

Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.

Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kituo cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.

Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.

No comments:

Post a Comment