Pages

Pages

Monday, August 12, 2013

Dina Cares wapata msosi na watoto yatima jijini Dar es Salaam

Mratibu wa hafla hiyo, Dina Marios kutoka Dada Dina Cares (pichani Mbele),akiwa sambamba na baadhi ya Wadau waliojitokeza kuifanikisha hafla hiyo ya chakula cha mchana na watoto Yatima kutoka vituo vitatu,kushoto ni  Dada  Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na wadau wengineo.
Mmoja wa Watoto akichorwa. 
 Mtangazaji wa Clouds FM, Dada Regina Mwalekwa na  Dada Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet wakiwa na baadhi ya watoto waliojumuika kwa chakula cha pamoja, kwenye hafla iliyohusu vituo vitatu vya watoto Yatima iliyofanyika kwenye fukwe ya Azula beach Kawe jioni ya leo.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kushoto ni Snura na kulia ni Shilole wakiwa na rafiki yao pichani kati wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja  na watoto.
Dada Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet akicheza mpira na watoto 
 Watoto wakipakuliwa chakula safi kabisa.
 Baadhi ya Wadau mbalimbali wakiwemo wasanii,wakiwasaidia watoto kuwaandalia chakula.
 Watoto waishio katika vituo vya kulelea watoto yatima na wengineo wakicheza michezo yo kwa pamoja.
 Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akiongea na Watoto kutoka vituo Yatima,kabla ya kukata keki na kuwalisha.
Mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares akimlisha keki mmoja wa watoto waishio katika mazingira Magumu kutoka kituo cha Watoto yatima cha Vetenari Temeke 
Baadhi ya watoto kutoka vituo vya watoto Yatima,kituo cha Sifa Bunju,Zaidia Sinza pamoja na Vetenari Temeke,wamekutana leo mchana kwenye Fukwe ya Azura Beach Kawe kwa ajili ya kupata chakula cha pamoja na watoto wengine,huku michezo mbalimbali kama vile face painting,jumping castle,kuogelea,kuvuta kamba,mpira wa miguu,kucheza mziki n.k.Michezo hiyo iliyoandaliwa na Kids Event na mingineyo ilitawala na kuwaburudisha sana watoto.
Aidha mratibu wa hafla hiyo,Dina Marios kutoka Dada Dina Cares,amesema kuwa mkusanyiko huo unafanyika kufuatia zoezi zima la kukamilisha ule mpango ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto yatima.

Pamoja na hafla hiyo pia Keki iliyoandaliwa na flying chefs  ilikatwa huku wasanii mbalimbali wakishiriki kwa pamoja,akiwemo Shilole,Snura,Quenn Darlin,Mwasiti na wengineo.Janet Sosthenes  Mwenda wa Ongea na Janet na Wasanii wengine walijitolea kuwahudumia na kuwaangalia watoto.
Dina Marios anawashukuru watu wote walioshiriki kuchangia vituo hivyo.Wadau wa blog yake www.dinamarios.blogspot.com wasikilizaji wa leo tena ya clouds fm na wote walioguswa. Mpango huo utaendelea siku nyingine tena maana ni endelevu

No comments:

Post a Comment