Pages

Pages

Tuesday, August 20, 2013

Rais Jakaya Kikwete akabidhi hati za Idhini ya Vyuo Vikuu vishiriki nane

Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Hati Idhini ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Nelson Mandera, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, wakati wa hafla ya kuvitunuku Hati Idhini Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, akimkabidhi Hati Idhini ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Nelson Mandera, Makamu wake, Prof. Burton Mwamila, wakati wa hafla ya kuvitunuku Hati Idhini Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Agosti 20, 2013. Katikati ni Rais Jakaya Kikwete, akishuhudia, na (kushoto) ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.

Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo.
Rais Jakaya Kikwete, akihutubia baada ya kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja na wakuu wa Vyuo hivyo Vishiriki.

No comments:

Post a Comment