Pages

Pages

Tuesday, August 20, 2013

Muumini, Waziri Sonyo wachapana makonde, pitia alichokisema kocha wa Dunia baada ya tukio hilo






Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WANAMUZIKI wawili wenye majina ya kutisha, Waziri Sinyo na Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamepigana katika mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.

Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.

“Leo ndio nimedhihirisha uyu ( hapa kuna tusi ila limefichwa kwa sababu za kiungwana) ni kweli yy amenikuta nimekaa tena pembeni na taadhali zote ila aluvyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe uyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu ndio ewe ewe wakamshika lkn wakati nakwepa kisu nilianguka kama sio George Gama ameshanijerui au kuniuwa kabisa ngoja nifunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa ili sina msalie mtume ivi jimwili lote la Sonyo Bado anashikia mwanaume mwenzie Kisu na amshuku Janurry alienipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikua kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kuipitia meseji ya Muumini.

Kupigana kwa wanamuziki hao ni muendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo.

No comments:

Post a Comment