Pages

Pages

Friday, August 30, 2013

Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni awalipua wapinzani

Na Rahimu Kambi, Handeni
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, amesema wananchi wengi wamegundua kuwa wapinzani hawana lengo zuri kwa maisha yao, ndio maana wanazidi kukiamini chama chao.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, wilayani hapa, Malunde alisema kwa sababu hiyo, wanaamini kuwa CCM itaendelea kuwa mkombozi kwa wananchi wote nchini.

Alisema mara kadhaa sera za viongozi wa upinzani zimeshindwa kujitosheleza, sanjari na kufanya mambo mengi ya kuwagawa Watanzania.

Aidha alijaribu pia kuzungumzia mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa wanachama wa CCM na Watanzania wote wanaendelea kuthamini mchango wa chama chao kwa kuongoza serikali kwa ajili ya kuwapatia maisha bora kwa kila Mtanzania.

“Tunashukuru kwakuwa wananchi wote wameelewa janja ya wapinzani na namna wanavyotaka kuwayumbisha Watanzania.

“Hili ni jambo jema kwa viongozi wote na ifikie wakati kila mtu aone namna ya kujiweka sawa na vyama vya upinzani, hasa kama kinachofanywa ni kuwachanganya Watanzania,”  alisema Malunda, ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment