Pages

Pages

Tuesday, August 13, 2013

Mdau wa muziki Yusuphed Mhandeni ajitosa kuwezesha mlipuko wa Cheza Kidansi Ijumaa ya Agosti 16




Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MDAU wa muziki na mfanyabiashara jijini Dar es Salaam, Yusuph Shaban maarufu kama Yusuphed Mhandeni roho ya nabii amejitolea kuudhamini mnuso na mlipuko wa Cheza Kidansi, uliopangwa kufanyika Agosti 16 mwaka huu katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Dalaam.
Yusuphed Mhandeni, pichani
Katika mlupuko huo, wahudhuariaji na wageni waalikwa wapata chakula safi kutoka kwa Chichi Catering, inayondeshwa na Karima ChiChi Mhandeni, mke wa Yusuphed.
Cheza Kidansi inavyoonekana pichani
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Yusuphed alisema kuwa ameamua kusaidiana na waandaaji ili wafanikishe mlipuko huo ikiwa ni pamoja na kusimamia masuala yote ya burudani.

Alisema kumekuwa na faida nyingi katika maatukio kama hayo, hivyo anaamini waalikwa wote watafaidika kwa kupata burudani sambamba na kujuana.

“Huu ni mlipuko wa cheza kidansi ulioandaliwa kwa sababu ya kufanya tathimini namna gani muziki wa dansi unaweza kupiga hatua na kutoka hapa tulipo sasa.

“Naomba kuwahakikishia kuwa kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa, maana chakula, burudani kutoka kwa Victoria Sound chini ya Mwinjuma Muumini watakuwapo,” alisema.

Mlipuko wa Cheza Kidansi umeasisiwa na mdau wa muziki wa dansi hapa nchini, Bernad James, anayefanya kazi ya utangazaji katika kituo cha Star Tv, jijini Mwanza Tanzania.

No comments:

Post a Comment