Pages

Pages

Tuesday, August 13, 2013

Kamati ya Uchaguzi kutangaza mchakato wa uchaguzi wa TFF kesho

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHAKATO wa uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa kesho (Agosti 13 mwaka huu).
Jamal Malinzi, pichani aligombea nafasi ya Rais wa TFF, uchaguzi ulioingia doa kabla ya kufutwa rasmi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Jumapili (Agosti 11 mwaka huu) na inatarajia kuwa na kikao kingine leo (Agosti 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itazungumzia maandalizi ya uchaguzi huo.

Mbali ya Mbwezeleni, wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana Manara.

No comments:

Post a Comment