Pages

Pages

Friday, July 26, 2013

Yanga wajivunia mazoezi ya kutetea ubingwa wao wa ligi ya Tanzania Bara

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema kuwa unaamini mazoezi wanayofanya wachezaji wao katika Uwanja wa Luyola, utawaweka katika nafasi nzuri katika michuano ijayo ya Ligi ya Tanzania Bara msimu ujao.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto
Ligi hiyo ambayo Yanga ndio mabingwa watetezi imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu 14 kuwania taji hilo.

Akizungumza mapema wiki hii, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema timu yao inafanya mazoezi kabambe kwa ajili ya kuwaweka sawa.

Alisema kwa kupitia uhodari wa kocha wao Ernest Brandit, wana amini mambo yatakuwa mazuri katika kuifanya timu yao itishe msimu ujao na kutetea vema taji lao.

“Timu yenye wachezaji wa ushindi wanafanya mazoezi yao katika Uwanja wa Luyola, huku tukiamini kuwa ubora wao utashangaza wengi.

“Lengo ni kutetea ubingwa wetu tuliyoutwaa msimu uliopita, hivyo kwa sasa majukumu yote yapo kwa benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla,” alisema.

Juzi katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki, Yanga walitoka sare dhidi ya timu ya URA ya nchini Uganda, ambayo walipocheza na Simba, waliibuka na ushindi wa bao 2-1.

No comments:

Post a Comment