Pages

Pages

Friday, July 26, 2013

DC Handeni aunga mkono juhudi za kuitangaza wilaya



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amewataka wadau na wananchi kuunga mkono juhudi za kuitangaza wilaya yao kwa kupitia watu mbalimbali, ikiwamo blog ya Handeni Kwetu.
Muhingo Rweyemamu, Mkuu wa wilaya Handeni.
Akizungumza hivi karibuni wilayani humo, Muhingo alisema kuwa juhudi zinazofanyika zinahitaji kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa, ili maendeleo yapatikane kwa vitendo.

Alisema hata kuanzishwa kwa blog ya Handeni Kwetu ni namna ya kuendeleza juhudi hizo kwa ajili ya kutafuta maendeleo kwa namna moja ama nyingine, jambo linalotia moyo.

“Wote tuendeleze juhudi za kuitangaza wilaya hii kwa nguvu zote, huku tukiunga mkono wale wanaojitolea, sambamba na kuanzishwa kwa blog ya Handeni kwetu hapa Tanzania.

“Naamini tukifanya hilo, hata wawekezaji wataendelea kuona mipango yetu mizuri, hivyo tusirudi nyuma katika kuwaza yale yenye manufaa kwa Handeni na Tanzania kwa ujumla,” alisema.

Blog ya Handeni Kwetu imekuwa ikijizolea mashabiki lukuki, jambo linaloongeza hamasa ya kuiweka kihabari zaidi na kuvutia watu mbalimbali kwa kuchanganya habari zote, bila kusahau makala za siasa na burudani.

No comments:

Post a Comment