Pages

Pages

Saturday, July 13, 2013

Wananchi 23,279 mkoani Kilimanjaro kunufaishwa na huduma ya maji safi



Na Kija Elias, Same
WAKAZI wapatao 23,279 katika wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro wanatarajia kunufaika na programu ya kitaifa ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP) unaotekelezwa na serikali katika halmashauri
zote hapa nchini.

Kukamilika kwa programu hiyo halmashauri ya wilaya ya Same inatarajia kupeleka huduma ya upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira  hususani katika maeneo ya mjini na vijiji ili wananchi hao waweze kupata maji ya uhakika kwa muda wote.


Gama akimtwisha mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Same kama ishara ya Uzinduzi.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akiwasili katika eneo la Mradi, kuzindua Mradi huo ambao uko chini ya Mpango wa RWSSP.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama Akizindua Mradi wa Maji kwa Vijiji vya wilaya ya Same ambapo zaidi ya wakazi 23,279 watanufaika nao ifikapo Juni mwakani.

Mmoja wa wakazi wa wilaya ya Same akiondoka na Maji baada ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Vijijini.

Nyumba hii.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akishiriki ujenzi wa Virura vya kutolea maji katika mradi wa Maji kwa Vijiji ambapo zaidi ya wakazi 23, 279 wanatarajiwa kunufaika ifikapo Juni Mwakani.
Mkuu wa Mkoa akikagua Matenki ya Maji katika Uzinduzi wa mradi wa Maji Vijijini chini ya Mpango wa RWSSP.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Same, Joseph Mkude alisema kuwa Halmashauri hiyo chini ya mpango wa programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini “RWSSP” imeanza kutekeleza programu hiyo ya kitaifa kwa vijiji kumi, ambapo kwa sasa halmashauri hiyo imejenga miradi mine.
 
Mkude aliyasema hayo jana wakati akitoa taarifa ya utekelezaji huo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama wakati alipokuwa akitembelea miradi ya maji wilayani humo.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kupungaza tatizo la maji kwa wakazi hao  ambao walikuwa wanakabiliwa na uhaba wa maji kwa muda mrefu na kuongeza kuwa wakazi hao 23,279 ambao wanatarajia kunufaika na maji hayo ni sawa na asilimia 9.

“Matarajio yetu ya wilaya baada ya kukamilika kwa miradi ya maji katika vijiji kumi tutaweza kuwahudumia jumla ya wakazi 23,279 ambao ni sawa na asilimia 9 ya wakazi wa wilaya ya Same, hii itapelekea huduma ya upatikanaji maji kuongezeka, kutoka asilimia 58 mwaka 2012/13 hadi kufikia asilimia 67 ifikapo june 2014”alisema Mkude.

Alisema vijiji ambavyo vilishaanza ujenzi wa miradi hiyo ni Myombo, Mteke, Sambweni na Mwembe na kwamba miradi hiyo yote imesha kamilia kwa asilimia 95.

Aidha aliongeza kuwa vijiji vinne kati ya kumi miradi hiyo ilishakamilika  na kwamba halmashauri hiyo inatarajia kuikabidhi miradi hiyo kwa wananchi ifikapo Julai 31 mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimasnjaro, Leonidas Gama alisema serikali kwa kutambua matatizo ya maji yanayowakabili wananchi wengi hapa nchini imetafuta fedha za ndani na nje ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi katika nchi nzima.

“Serikali ilikuwa inalitambua tatizo la maji safi kwa wananchi wetu, hivyo serikali imeleta mpango wa kuwapatia vijiji kumi kila wilaya hapa nchini ili ifikapo 2014 tatizo la maji litakuwa historia tena” alisema Gama.

No comments:

Post a Comment