Pages

Pages

Saturday, July 13, 2013

MAMBO FULANI MUHIMU: Umagharibi usivunje maadili ya familia



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KADRI muda unavyokwenda mbele, ndio kukua kwa Sayansi kunazidi kuchanja mbuga kutokana na wataalamu kuumiza vichwa kuwaza na kuwazua kwa ajili ya kuvumbua vitu mbalimbali duniani.
Utamaduni huu sio wa Tanzania japo jamii ya nchi yetu imekuwa ikiweka mkazo sana katika masuala ya urembo kama inavyoonekana pichani.

Kila mtu anawaza namna gani ya kuvumbua ugunduzi wake, jambo ambalo kwa wenzangu na mimi tunatumia nafasi hiyo kufanya vitu hata yale yasiyokuwa na tija kwetu.


Na ndio hapo baadhi yao wanapoishi tofauti na maadili yao, huku wengineo wakijifanya ni Wazungu, jambo ambalo linachangia kuvuruga uhalisia wao wa kimaisha.

Wapendanao kama kawaida.
wa bahati mbaya, Tanzania ni kati ya nchi ambazo watu wake wamejiingiza zaidi katika Umagharibi na kulifanya Taifa lipate hasara kwa kuzalisha vizazi visivyojali Utamaduni wao.

Ndugu msomaji wangu, wapo wazazi wanaoshi na watoto wao kama watu baki na sio watoto wao wa kuwazaa.

Ni pale binti anapokaa sebuleni na nguo fupi ya kubana, tena akikaa upande mmoja, huku sehemu kubwa ya mwili wake ukibaki wazi, hivyo kuwa mbaya sana.

Mbali na mabinti hao, pia wapo baadhi ya akina mama wanatembea ndani ya nyumba huku wakiwa wamevaa nguo zenye kuonyesha sehemu za mwili wao.

Hali hiyo inasababisha kuchochea matamanio ya watu wengine hata wale wasiostahili pamojaa na kuvunja utu na maadili ya Watanzania.

Tanzania imekuwa ikikumbwa na vitendo viovu, hasa vya watoto kujihusisha kimapenzi na wazazi wao, ingawa si wote wanaoishi kwa mtindo huu katika jamii.

Mara baada ya penzi hilo kuanzishwa, hushindwa kuvunjika kwa haraka, hadi hapo mabaya zaidi yanapojitokeza.

Katika jamii yetu hii, wapo wakina baba ambao hadi kesho wanatembea na watoto wao, yani kuwa wapenzi wao. Mbaya zaidi, akina baba hao huwafanyia vituko wake zao, ili wapate nafasi ya kujinafasi na watoto wao huku wakijua mtindo huo si wa kiungwana.

Lakini haya yamesababishwa na sisi wenyewe. Mtoto hawezi kubaki sebuleni na kichupi, matiti yake yote nje, akizungumza na baba yake au mwingine yoyote nyumbani kwao.

Mtoto wa kike, hasa wale wanaoanza kuingia kwenye balehe, lazima ajiheshimu kwa kuhakikisha kwamba mwili wake unalindwa na kufichwa kadiri inavyowezekana.

Wakati wakikaa sebuleni na vivazi vya ajabu, pia hufikia mbali zaidi wanapotoka out wote. Hapo utawakuta wakicheza kwenye fukwe, huku baba akiwa na bukta na mtoto wake kichupi.

Matiti yake yapo nje na robo tatu ya miili yao ipo wazi. Kwanini? Ndio utandawazi huo unaokuja kwa kuvuruga utu wetu? Kuna kila sababu ya jamii kuanza kuangalia tamaduni zisizokuwa na mashiko.

Si kila jambo la Wazungu linafaa kuigwa na sisi. Tusijidanganye jamani. Yapo mambo mengi ambayo kwetu sisi ni mazuri, maana Tanzania ni nchi ya kujiheshimu kwa watu wake.

Sisi si watu wa kutembea uchi. Ule mtindo wa kufanya mambo kinyume ni lazima uachwe kama kweli tunahitaji kujisawazisha hapa tulipofikia leo.

Sina lengo la kuwakata wazazi kuwa karibu na watoto wao, ila ni kuacha yale yenye kuleta matusi kwa wana jamii hao. Kwani bila kumvalia baba yako kichipi ndio thamani yenu hutoweka?

Kwani ni lazima kuvaa chupi unapozungumza na mtoto wako? Hayo ndiyo mambo ya kuiga. Si mazuri hata kidogo.

Ni aina ile ile ya ulingo huu, ingawa si mzuri unaofaa kuachwa haraka iwezekanavyo, ndio maana nimeamua kuiweka nikiamini kwamba tutaendelea kukosoana.

Lazima ijulikane baba na mtoto kwa ajili ya kuwafanya wasisababishe mwingiliano hata kwa wale wanaopenda kuishi kama Wazungu majumbani mwao.

Inapotokea wamekaa sebuleni pamoja, basi kila mmoja ajichunge ili asilete nidhamu mbaya kwa mwingine.

Hayo si maisha yetu, japo Dunia ya leo imekumbwa na balaa la kuona kuwa kila mtu ana haki ya kujifanya hana haya kwa yoyote, akiwapo baba na mtoto na kujiachia ovyo ovyo tu.

+255 712 053949


No comments:

Post a Comment