Pages

Pages

Monday, July 01, 2013

Wakati Rais Barack Obama akiingia leo Tanzania, fahamu kidogo alipotokea kabla ya kupata mafanikio ya kuongoza Taifa la Marekani

WAKATI Rais wa Marekani, Barack Obama anawasili leo akitokea nchini Afrika Kusini katika ziara yake ya nchi tatu za Afrika ikiwamo Senegal, Afrika Kusini na Tanzania akiingia leo mchana, rais huyo amekula msoto kabla ya kufikia mafanikio yake.
Rais Barack Obama wakati huu.
Wachache wanaweza kusema rais huyo amepata raha kuanzia mwanzo hadi leo anaishi akiwa na mafanikio makubwa, hususan ya kuongoza Taifa kubwa la Marekani.

Obama anasema,  " Wakati tukiendelea na masomo yetu ya Sheria mimi na Michelle tulifanya kazi katika kampuni ya Uwakili ya Sidley na Austin jijini Chicago.
 
Binafsi nilikuwa na wasi wasi kuhusu ujana wangu na hasa changamoto kuwa maisha ya sasa ni fedha. Hofu yangu ilikuwa ni lini nitaanza kukamata fedha nyingi ili zisaidie mawazo na fikra zangu kufikia mahala ninapotaka.

Obama enzi hizo.
Lakini, kutokana na kupanda kwa gharama na mkopo niliyochukua Serikalini kwa ajili ya masomo, niliamua kuendelea kuwatumikia mabwana wawili; chuo na kampuni ya sheria.

Nilijitahidi kadiri nilivyoweza kundunduliza sehemu ya kipato changu . Hatimaye nilifanikiwa kuwa na chumba. Nilinunua suti zangu tatu na pia jozi moja ya viatu.

Hata hivyo, wakati nanunua viatu sikuwa makini, kwani vilionekana vidogo; vilivyonibana na kunifanya nionekane mshamba. Siku niliyopiga ripoti ofisini, kila mmoja aliniangalia.
Ingawa sikujua ni kwa nini, lakini nilihisi walifanya hivyo kutokana na viatu vyangu!"- Barack Obama.

No comments:

Post a Comment