Pages

Pages

Saturday, July 06, 2013

Wafanyabiashara Manzese wapigwa mabomu ili wasirudi katika maeneo yao baada ya kumpisha Rais wa Marekani, Barack Obama



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAKAZI na wananchi wa Manzese jijini Dar es Salaam, mchana wa leo ulikuwa mchungu kwao katika fujo zilizosababisha kurushwa kwa mabomu dhidi ya wafanyabiashara waliokuwa wamejerea katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Daraja maarufu la Manzese jijini Dar es Salaam
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuondoka kwa Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye ziara yake Tanzania ilisababisha kuhamishwa kwa wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Shuhuda wetu alisema kuwa pilika pilika hizo za mabomu ya Askari Polisi waliokwenda kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawarudi katika eneo la Manzese.

“Hali ilikuwa mbaya mno ambapo pia kurushwa kwa mabomu kulisababisha kuzua kwa taharuki ya aina yake na baadaye kusababisha foleni kubwa kwa gari zinazotumia barabara ya Morogoro,” alisema.

Mara baada ya Obama kurudi kwao Marekani, wafanyabiashara ndogondogo wamerudi tena katika vijiwe vyao kuendelea na biashara zao, ambapo serikali ya jiji imesema itahakikisha kuwa watu hao hawarudi tena katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Sadick, alisema jana kuwa suala la kuwabana wafanyabiashara hao wasirudi katika maeneo yasiyoruhusiwa ni jambo la lazima pamoja na kulitunza jiji kutokana na uchafu.
 

No comments:

Post a Comment