Pages

Pages

Monday, July 15, 2013

Waandishi wa habari waaswa kutenda haki



Na Kambi Mbwana, Handeni
WAANDISHI wa Habari hapa nchini wameaswa kuandika habari kwa haki kwa kuelezea mabaya na mazuri ili jamii iendelee kuishi kwa heshima ndani na nje ya nchi.
Salum Masokola, Katibu wa Mbunge Abdallah Kigoda, Handeni.
Hayo yalisemwa leo na Salum Masokola, Katibu wa Mbunge wa Handeni, mkoani Tanga, Abdallah Kigoda, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

Akizungumza na Handeni Kwetu Blog ofisini kwake, Masokola alisema kuwa kuna baadhi ya waandishi wanachoweza kufanya wao ni kuelezea mabaya tu na kuacha mazuri.

Alisema waandishi wa aina hiyo ndio wale wanaosababisha mtafaruku kwa jamii hususan kwa viongozi wanaoandikwa bila kuangalia mazuri yao waliyofanya kwenye jamii.

“Hali hii inasababisha baadhi ya watu kuona kuwa serikali haijafanya mazuri wakati si kweli, hivyo kuna kila sababu sasa ya waandishi kukaa kwenye haki.

“Wakifanya hivyo mambo yatakuwa mazuri maana jamii itaishi kwa heshima na kuleta maendeleo yao kwa kushirikiana na viongozi wao sehemu mbalimbali za Tanzania,” alisema Masokola.

Wilaya ya Handeni ni miongoni mwa zile zinazopigania maendeleo ya wananchi wake, huku kwa sasa ikiwa chini ya Mkuu wake wa wilaya, Muhingo Rweyemamu.

No comments:

Post a Comment