Pages

Pages

Monday, July 22, 2013

Vyama vya upinzani vyalaumiwa wilayani Handeni


Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
ALIYEKUWA mgombea udiwani wa Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni mkoani Tanga, kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Mwamini Andrew, amesema hali ya siasa inavyokwenda, ni ngumu kwa vyama vya upinzani, kikiwamo CUF kufanya vizuri katika wilaya ya Handeni.
Mwamini Andrew, aliyekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Kwamatuku mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF.

Mwamini aliyasema hayo katika mazungumzo marefu na Blog ya Handeni Kwetu kijijini Komsala, akielezea pia mikakati yake kisiasa kwa ajili ya kuliletea maendeleo Taifa lake.

Mwanasiasa huyo chipukizi alisema kuwa vyama vya upinzani vingi vinaelemea sana sehemu za mjini, huku wakishindwa kubuni mipango ya kuwakomboa watu wa vijijini.

Alisema suala hilo lilisababisha CUF lishindwe kutambua mchango wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 licha ya kuwa mgombea udiwani pekee katika wilaya ya Handeni aliyepata kura nyingi, licha ya kuangushwa na diwani wa CCM.

“Hizi ni changamoto kubwa ambazo huenda zikaangamiza siasa za Tanzania, maana vyama vingi vya upinzani vinaona mjini ndio kila kitu, wakati wananchi wengi wapo vijijini.

“Jambo hili ndilo lililofanya CUF washindwe kutambua umuhimu wangu pamoja na wengine wote, hivyo huenda likazua kinyongo kwa uchapakazi wa sisi wawakilishi wao,” alisema.

Katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, chama pekee kinachokubalika kwa wananchi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikifuatiwa na CUF ambacho hata hivyo kinaonekana kupoteza thamani yake machoni mwa wananchi wengi wilayani humo.

No comments:

Post a Comment