Pages

Pages

Sunday, July 21, 2013

Super D aachia DVD mpya za mapigano kuendeleza mchezo wa masumbwi


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa mchezo wa masumbwi hapa nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’, amesema kuwa kitendo cha kutengeneza DVD za ngumi ni hatua yake ya kuhakikisha kuwa vijana wanajifunza masumbwi.
 


Kazi za Super D zilizoingia sokoni.
Alisema anaamini kuwa wengi wanaobahatika kuona CD hizo wana uwezo wa kupata mwangaza na mahitaji ya kujikita zaidi katika mchezo wa masumbwi na hatimae kufikia malengo yao waliyojiwekea.

Alisema kitendo cha bondia chipukizi kuwa na muda wa kukaa na kujifunza ngumi kwa kuangalia waliyompita kiwango ni jambo lenye kutia moyo katika harakati za mchezo wa masumbwi duniani.

Super D alisema suala hilo anaamini litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa njia nzuri wadau wa ngumi wakiwamo mabondia chipukizi wenye malengo ya siku moja kuwika katika sekta ya mchezo wa ngumi duniani.

“Nimekuwa nikitengeneza CD mbalimbali ambazo kwa kiasi fulani naamini zina uwezo mkubwa wa kuwapatia mwangaza vijana wote na wale wanaopenda kufuatilia mchezo huo hapa nchini.

“Tayari nimekamilisha toleo jipya la CD za ngumi na wadau wote wanaweza kuzipata sehemu mbalimbali, hususan katika makutano ya Uhuru na Msimbazi au Jengo la Azam lililopo karibu na Kituo cha Polisi Gelezani,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Super D, DVD hizo zimejumuisha mapambano ya mabondia wenye uwezo wa kurusha masumbwi, akiwamo Mike Tyson, Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones, Miguel

No comments:

Post a Comment