Pages

Pages

Sunday, July 21, 2013

Handeni wahaha na uhaba wa walimu wa sekondari



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
AFISA Taaluma Shule za Sekondari wilayani Handeni, Basil Mrutu, amesema wilaya yao ina walimu 376, wakati mahitaji ni 666, hivyo kusababisha ugumu katika malengo yao ya kukuza kiwango cha elimu na ufaulu katika wilaya hiyo.
Basil Mrutu, Afisa Taaluma wa Sekondari wilayani Handeni.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog wilayani hapo juzi, Mrutu alisema kuwa upungufu huo unawafanya walimu waliopo washindwe kuwamudu wanafunzi kwa shule zilizopo wilayani kwao.

Alisema kuna kila sababu ya serikali kuwaongezea walimu ili juhudi za kunyanyua kiwango cha elimu na ufaulu kwa ujumla wilayani kwao kuongezeka.

“Tunahitaji walimu kwa ujumla, maana waliopo sasa ni 376 tu, wakati mahitaji kamili ni 666, hivyo kiwango hiki ni kidogo kulingana na mahitaji ya shule katika wilaya yetu.

“Naamini tukifanikiwa juu ya suala hilo, harakati zetu za kuongeza kiwango cha elimu wilayani kwetu kitaongezeka, maana walimu watakuwa wanakidhi mahitaji kamili kwa shule zote za sekondari,” alisema Mrutu.

Aidha Mrutu alisema mahitaji ya walimu wa Sayansi wilayani humo ni 100, wakati waliopo sasa 58 kati ya 158 wanaohitajika kufundisha katika shule za sekondari zilizopo kwenye wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment