Pages

Pages

Sunday, July 07, 2013

Pitia kauli ya Mwalimu Nyerere juu ya milima na mabonde ya kuulinda Muungaano wa Bara na Visiwani



KATIKA kuelekea kuipata Katiba Mpya, kumekuwa na maneno mengi na mitazamo kutoka kwa watu tofauti katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yani Bara na Visiwani.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekaa kushoto akiwa na Sheikh Abeid Aman Karume enzi za uhai wao na wakilitumikia Taifa.
Kubwa zaidi ni Katiba Mpya itamke wazi serikali tatu, jambo ambalo upande mwingine hauungi mkono kwasababu ni mwelekeo mbaya wa Muungano wetu wa Bara na Visiwani.

Katika kupekua pekua kauli za waasisi wa Muungano huu, Hayati Baba wa Taifa, aliwahi kutolea ufafanuzi suala la Muungano na kusema kama ifuatavyo.

"Ni ulevi tu hasa ulevi wa madaraka mnanchi moja mnaleta leta mambo ili
kuvunja muungano mpate sehemu nyingi zaidi za kuongoza n ulevi tu.
Wakat tunaunganisha nchi hizi Karume alinambia (Serikali moja na wewe Nyerere rais) nikamwambie sheikh Zanzibar muwadogo nyie mtapoteza utambulisho wenu

Tukakubaliana tuwe na muungano wa aina yake duniani ambao Zanzibar watakuwa na serikali yao kwa mambo ya Zanzibar

Ukiwasikiliza Zanzibar utakubali kuwa tungalikuwa na serikali moja wakati ule wangetokea watu wakutaka kujitenga haraka na ndio mana hoja zao zote leo zinathibisha niliyomwambia Karume wakati ule juu ya utambulisho wa Zanzibar sasa wanao wanatafuta nini watu hawa.

Kwakuwa bara ni kubwa zaid kwa watu na jiografia serikali yake itakuwa ni
serkal ya muungano ambayo itahusika na mambo yote ya bara na yale ya muungano

Utaratibu huu umetusaidia hapa tulipofka taifa la amani na udugu wa mfano duniani

Viongozi muwe wakali kulinda Muungano huu kwakuwa wapingaji watakuwapo tu! Akitokea kiongozi anadhamira yakutugawa afungiwe pahala atulie tu aone kama kutengwa kunamsaidiaje.

Basi wakati ule wakaanza kujitokeza watu ambao wanaona hawakubaliki znba na wanataka urais wakaona hapa tanganyika ikiwa na serkal yake tunaweza kuongoza (watu wa ovyo hawa mana ata hilo jina tanganyika mm sijuhi limetokea wapi?

Nimetafuta sana sijajua na silipendi kwakuwa tulibatizwa na wanyonyaji. Na kule Zanzibar wakawepo watu wanataka kuongoza hawakubaliki bara
wakafikiri kukiwa na serikali ya nchi bila bara watakuwa marais na jeshi na Bendera na nini na nini.

Huu ni uroho tuu hasa uroho wa madaraka CCM na Watanzania watakuwa
wanafanya makosa sana wakikataa aina hii ya muungano wa serikali mbili kwa sababu wanazotengeneza kila kukicha. Tukayaweka hayo kwenye katiba ya 1977.

Wapuuzi hawakosekani tu watakuwapo ata mkiwa na serikali 4 watataka 5
mtakuta mwisho mnaserikali ya Kaskazini mana wapo watu wanatamani hilo” Mwisho wa kunukuu. Je, haya yanatokea sasa mwisho wake nini katika kuifanya Tanzania ibaki salama?



No comments:

Post a Comment