Pages

Pages

Sunday, July 07, 2013

DC Handeni awataka Polisi wawe mfano bora mbele ya jamii


Na Mwandishi wetu Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Muhingo Rweyemamu, amewaagiza Wastaafu wa Jeshi la Polisi nchini kudumisha nidhamu waliojengewa wakiwa ndani ya Jeshi hilo hata watakapokuwa Uraiani ili kuwa mfano mbele ya Jamii.
Katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Tawala wa Wilaya ya Handeni Pendo Magasha, pichani aliyesimama, Muhingo alisema kwa muundo wa Kijeshi, kila Askari ni mtu mwenye nidhamu na hivyo kama atafanikiwa kufanya kazi na kustaafu kwa hiyari ni wazi kuwa mtumishi huyo atakuwa mfano kwa wengine kwa hivyo wakawe tena mfano kwa watu watakaoishinao huko Uraiani.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Amewataka kwenda kuwa mabalozi wema waendako kuishi na watu wengine na kwamba ipo haja ya Wastaafu kusaidia kutoa elimu sio kwa wenzao wanaobaki kazini tu lakini pia hata kwa wananchi wengine hasa vijana watakaokwenda kuishi nao ili kujenga familia zenye maadili mema.

Awali Mkuu wa Polisi Wilaya ya Handeni SP. Zuberi Chembera, akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Constantine Masawe, alisema kuwa kutokana na utandawazi uliopo kwa sasa kuna haja ya Polisi wanaobaki kazi kubadilika kimatendo na kwenda sambamba na mfumo uliopo huku kila mmoja wao akizingatia maadili na kuwahudumia wananchi kwa upendo na ukarimu kuliko ilivyo zamani.

Naye mmoja wa wastafu hao, Meja Jumbe Mohammed Saidi, akitoa shukrani, aliwataka wenzake wanaobaki kazini kila mmoja kwa nafasi yake, ni lazima atoa huduma bora katika kuwahudumia wananchi wanaofika vituoni kuomba msaada kwa vile siku hizi kila mtu anajua haki zake.

Amesema kama mwananchi atafanyiwa kinyume na matarajio yake ni lazima atalalamika na hataona kama aliyekwenda kinyume ni mtu mwenyewe bali atapeleka lawama kwa Jeshi zima la Polisi na kuwaona kuwa wote hawatendi haki kwa wananchi.

Katika hafla hiyo, Wastaafu hao walipewa zawadi mbalimbali zikiwa fedha taslimu pamoja na mabadi 25 kwa kila mmoja huku Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Vibaoni wilayani humo Mw. Abdi Kipacha, akiwachangia Askari hao mabati 15huku akisema kama bila ya Askari Polisi hakuna usalama na hivyo hata yeye kazi yake ya Uwalimu asingeweza kuifanya vizuri kwa vile watoto wahawatakwenda shuleni kama hakuna amani.

Wastaaru walioagwa ni Inspekta Xavery Chaula na Meja Jumbe Mohammed Saidi waliolitumikia Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 35 kwa kila mmoja na Meja Gabinus Nyoka aliyelitumia Jeshi hilo kwa muda wa miaka 36.

No comments:

Post a Comment