Pages

Pages

Wednesday, July 24, 2013

Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu atangaza neema wilayani humo



Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
MKUU wa wilaya ya Handeni, amesema kuwa katika uwapo wake katika wilaya hiyo, atahakikisha rasilimali nyingi zilizokuwapo hapo zinawanufaisha wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani humo, Muhingo alisema kuna baadhi ya neema zilizoanza kuonekana baada ya kufanyiwa utafiti, yakiwamo madini ya kutengeneza chuma.

Alisema endapo mpango huo utafanikiwa kama utakavyopangwa, basi lazima kiwanda cha kutengenezwa kiwapo wilayani humo kwa ajili ya kuzalisha ajira pia kwa Watanzania wote.

DC Muhingo alisema hatakubali kuona wawekezaji hao wanatoa rasilimali hiyo na kuipeleka katika nchi zao na baadaye kuwaletea Watanzania na kununua kwa bei ghali.

“Sitaki kusema yote yanayoonekana katika wilaya hii, maana ni vingi mno na utajiri mkubwa, yakiwamo madini haya ambayo yakitumiwa vizuri Taifa litazidi kusonga mbele.

“Tumeshasema na wenzetu kuwa kama kweli kunahitajika kuchimbwa kwa madini hayo, basi na hicho kiwanda kijengwe katika wilaya hii ili iwe chanzo cha ajira kipya,” alisema.

Wilaya ya Handeni kwa sasa inategemea kilimo na ufugaji, huku changamoto zilizopo ni mabadiliko ya Tabia Nchi yanayosababisha wakulima wapate msoto katika kazi zao.

No comments:

Post a Comment