Pages

Pages

Thursday, July 18, 2013

Kituo cha Watoto yatima cha Islamic chaomba msaada kwa wasamaria wema



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KITUO cha watoto yatima cha Yatima Islamic, kinaomba msaada kwa wasamaria wema kukisaidia pango la nyumba.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kituo hicho kilichopo Buguruni Ally Hamza, Rashid Akungwa alisema kuwa, wanadaiwa pango zaidi ya sh. milioni nne, baada ya awali waliyolipiwa na mhisani kuisha muda wake.

"Awali alijitokeza mtu ambaye, aliona mazingira ya watoto, kwamba tulikuwa katika nyumba ya vyumba viwili, na watoto ni wengi..ndipo alipotutafutia sehemu hii na kutulipia kodi ya mwaka ambayo imeshamalizika tangu mwezi uliopita,"aliongeza.

Alisema kwa sasa wana hali mbaya, na endapo watafukuzwa katika nyumba hiyo, basi watoto hao zaidi ya 50, huenda wakakosa pa kwenda na hatimaye kuzagaa mitaani.

Watoto wengi wanaoishi katika kituo hicho wana umri kati ya miaka minne hadi 15, ambapo wengi wanasoma shule ya msingi, huku mmoja aliyekuwa akisoma sekondari, amemaliza.

Katibu wa kituo hicho, Aboubakary Simba, alisema mahitaji mengine ni pamoja na futari na daku hasa kwa mwezi huu wa Ramadhani, mavazi kwa ajili ya watoto na mahitaji ya kawaida ya kibinadamu.

Alisema msaada wa aina yeyote wenye hadhi na utu, unapokelewa na kwa yeyote ataliyeguswa kuchangia anaweza kupata maelezo kupitia namba 071 03 8888 au 0712150928.

No comments:

Post a Comment