Pages

Pages

Friday, June 28, 2013

Wazabuni wakutana jijini Dar es Salaam leo kujadili changamoto zao



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZABUNI leo wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali katika kazi zao.
Engineer James Dotto kutoka Kampuni ya SimbaNet (T) Ltd, akizungumza jambo katika kikao cha pamoja cha Wazabuni kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia changamoto wanazokutana nazo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Ununuzi na Ushauri wa Government Procurement Services Agence (GPSA) Yoswam Nyongera, huku kikiandaliwa na mratibu wake Francis Mugasa.
 Mkurugenzi Ununuzi na Ushauri wa Government Procurement Services Agence (GPSA) Yoswam Nyongera, akizungumza jambo katika kikao cha Wazabuni kilichofanyika leo. Kulia kwake ni Mratibu wa kikao hicho, Francis Mugasa.


Mratibu wa kikao hicho, Francis Mugasa.
 Wadau wa Zabuni wakifuatilia kwa umakini kikao chao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Wadau wakijadiliana jambo juu ya mambo ya Zabuni.
Katika kikao hicho, wazabuni hao walikuwa wakielezea changamoto wanazokutana nazo, yakiwamo ucheleweshwaji wa malipo yao wanayokutana nayo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Nyongera alisema kuwa juu ya ucheleweshwaji wa malipo kunatokana na taratibu za kisheria, hasa kukaa siku 30 baada ya kumaliza kazi ndipo mzabuni afuatilie malipo yake.

“Malipo ni haki ya Mzabuni mara baada ya kufikia makubaliano ya kazi ambazo wamefanya na serikali.

“Hakuna taasisi ya serikali inayoruhusiwa kutangaza tenda za Zabuni kwa wazabuni kabla hajajua watapata wapi fedha za kumlipa mzabuni huyo,” alisema.

Kila mmoja alitoa dukuduku lake, ambapo Mkurugenzi Nyongera aliyasikiliza na kuyatolea ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment