Pages

Pages

Tuesday, June 04, 2013

Watu washindwa kuzuia vilio vyao katika mapokezi ya Ngwea Uwanja wa Ndege



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WATU wengi walijitokeza leo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini, Jumanne ya wiki iliyopita.
Wadau wakijiandaa kuupokea mwili wa Ngwea Uwanja wa Ndege, huku kila mmoja akiwa haamini kinachotokea, huku Polisi nao wakiwa tayari kulinda usalama.
           Msanii Keisha akiwa haamini macho yake.
                           Kalale pema peponi Kamanda Ngwea
 Jeneza la Ngwea likibebwa tayari kupakiwa kwenye gari la kuelekea Hospitali ya Taifa, Muhimbili

                   Kila mmoja akilia kivyake
 Watu wakilia katika mapokezi ya mwili wa Ngwea
Mrisho Mpoto naye alikuwapo
 Huyu naye alibambwa uwanjani hapo akidaiwa kutaka kumkwapulia msanii TID katika pilika pilika za mapokezi ya mwili wa msanii Albert Mangwea.
 Gari lililobeba mwili wa marehemu Ngwea likijiandaa kuelekea Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Mwili huo unaagwa kesho Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Ndugu wa marehemu Albert Mangwea, wakiwa na uso wa huzuni wakipokea mwili wa Ngwea.

Mwili huo leo umehifadhiwa tena katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati kesho kuanzia saa mbili asubuhi utaagwa katika Viwanja vya Leaders Club, wakati saa sita mchana mwili huo utapelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika siku ya Alhamisi.

Umati wa watu ulifurika katika Uwanja wa Ndege, huku majonzi na vilio vikishika hatamu kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuupokea mwili huo. Wasanii wengi wa muziki walifika uwanjani, akiwapo Mrisho Mpoto, Madee, Fid Q, Keisha, Profesa Jay na wengineo.

No comments:

Post a Comment