Pages

Pages

Wednesday, June 05, 2013

Mamia wamuaga Ngwea Leaders Club, wasanii wajazana, mwili wake wasafirishwa Morogoro, kuzikwa kesho



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Marehemu Albert Mangwea ameagwa leo katika Viwanja vya Leaders Club na kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika kesho katika Makaburi ya Kihonda.
 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba kushoto akijadiliana jambo na viongozi wa Kamati ya Mazishi katika shughuli yaa kumuaga marehemu Albert Mangwea, katika viwanja vya Leaders Club leo.

Wasanii wanaaga sasa.

 
 Mbunge Idd Azzan anamuaga Ngwea

 Watu wanamlilia Ngweaa
 Sehemu ya waombolezaji waliokwenda wakimuaga marehemu Ngwea katika viwanja vya Leaders Club leo.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa Chadema (BAVICHA), John Heche wa tatu kutoka kushoto akijadiliana na viongozi wenzake waliokwenda kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea leo viwanja vya Leaders Club leo.
 Fid Q na Feroos wakibadilishana mawazo katika viwanja vya Leaders Club leo.
 Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan kulia, akijadiliana jambo na mjukuu wa Julius Kambarage Nyerere, Sofia Nyerere na ndugu yake kushoto kwake katika viwanja vya Leaders Club leo.
 Waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakijadiliana jambo katika viwanja vya Leaders Club leo.
 Sehemu ya waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakionekana katika viwanja vya Leaders Club leo.
Sehemu ya waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea ikiwa kwenye pilikapilika za kutaka kumuona kwa karibu msanii Diamond, hivyo kuvunja utaratibu mzima, wakati shughuli hiyo inaelekea mwishoni katika viwanja vya Leaders Club leo.

Idadi kubwa ya wasanii na mashabiki wao walihudhuria katika tukio zima la uagaji wa marehemu Ngwea.

Aidha viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa walihudhuria katika viwanja vya Leaders Club, wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzam.

Msanii Nassib Abdulmalick ‘Diamond’ alimuelezea marehemu Ngwea kama moja ya wasanii wenye uwezo mkubwa wa kuimba, huku akiweza kuishi kwa upendo na wasanii wote, tangu alipojiingiza kwenye muziki.

“Nimeguswa sana na msiba wa Ngwea, naamini pengo lake haliwezi kuzibika, maana jamaa alikuwa na uwezo mkubwa mno katika tasnia hii, akitamba na nyimbo nyingi zilizowafurahisha watu wote,” alisema Diamond.

No comments:

Post a Comment