Pages

Pages

Tuesday, June 25, 2013

Watoto yatima wa Ngeze Education Center kujumuika na wenzao katika Tamasha la Raha za jana na leo

 
Watoto yatima wa kituo cha Ngeze education center kilichopo maeneo ya kinondoni kwa  msisiri watajumuika na watoto wenzao katika tamasha la Raha za jana na leo linalojumuisha burudani ya bendi za muziki wa dansi, huku likifanyika Julai 6 katika Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Wasanii nguli wa filamu na bongoflava wanaokubalika kwa watoto watakuepo kula,kuimba na kucheza na watoto wote watakaodhulia katika tamasha hilo amabapo kiingilio kwa watoto wadogo kitakuwa ni bure ambapo wazazi wao watalipa kiasi cha tshs 8,000 tu.



Jumla ya bendi sita zitapanda jukwaani moja kuonyesha ukali wake,pia zile nyimbo mpya kutoka katika bendi hizo utazisikia zikipigwa live,bendi hizo ni Twanga Pepeta"African Stars",Mashujaa musica Band ikiongozwa na Chalz baba " wazee wa tuzo tano",Bantu group ikiongozwa na   ikiongozwa na "komandoo Hamza kalala".



Bendi zingine ni King kikii"wazee sugu",OTTU jazz band"MSONDO",King Kikii "wazee sugu" na DDC Mlimani park "SIKINDE" tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika viwanja vya posta vilivyopo kijitonyama jijini Dar es salaam.
 Milamgo ya viwanja hivyo itafunguliwa saa tano asubuhi ambapo michezo ya watoto itaanza na kuisha saa kumi na mbili jioni ambapo burdani za bendi zikiendelea mpaka usiku wa manane.

No comments:

Post a Comment