Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
VIONGOZI wa matawi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), wameaswa kufanya kazi zao kwa umakini na uangalifu katika
kuhakikisha kuwa chama chao kinaendelea kupendwa na Watanzania.
Calist Lyimo akizungumza katika semina hiyojanaSemina ya CCM jana ilikuwa poa
Wana CCM Makumbusho wakiwa kwenye semina jana.
Hayo yamesemwa na Katibu wa
Uenezi wa CCM, wilaya Kinondoni, Mwinyimkuu Sangalaza, katika semina
iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Kata ya Makumbusho, ambapo pia
ilifunguliwa na MNEC wa CCM Kinondoni, Calist Lyimo.
Akizungumza na viongozi wa
matawi hayo katika semina hiyo,
Sangalaza, alisema kuna haja ya viongozi wa matawi hayo, ambao ndio mhimili wa
chama kufanya kazi kwa umakini na kukipigania zaidi na zaidi katika harakati za
kisiasa nchini.
Alisema Tanzania kwa sasa
inakabiriwa na changamoto nyingi za kiuongozi, hasa kwa kuona baadhi yao
wanafanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wenye pesa na kuendeleza fitina.
“Sisi tupo ndani ya CCM, lakini
hatuna mchango wowote maana wengi wao tunapenda chuki na kuweka visasi dhidi ya
wenzetu, hivyo ufanisi unakuwa mdogo katika kazi zetu.
“Naomba tuache hayo kwa ajili
ya maslahi ya CCM katika kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka
2014 na ule Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015,” alisema.
Katika semina hiyo, watoa mada
walikuwa ni Holestes Damino, Muhidin Said, Ibrahim Hella na Sangalaza, mara
baada ya kufunguliwa na MNEC, Lyimo, wakati walioandaa ni Kata ya Makumbusho
kwa kupitia viongozi wao Hashim Athuman, Fatuma Sadiki, Abdi Abbasi Haidery
Suwea, chini ya uratibu wa Mchumi wa Kata ya Makumbusho, Yusuph Shaban Mhandeni
kwa maslahi ya CCM.
No comments:
Post a Comment