Pages

Pages

Sunday, June 30, 2013

Twanga Pepeta kuizundua albamu yao ya Nyumbani ni Nyumbani leo Leaders Club

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZEE wa Kisigino, bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”  leo Jumapili inazindua albamu yake 10 ijulikanyo kwa jina la ‘Nyumbani ni Nyumbani’, katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, sambamba na kusherehekea miaka 15 tangu kuanzishwa kwake.
Mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu.
Uzinduzi huo utapambwa  na michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET Bonanza.
Timu hizo zitaongozwa na ile ya waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point, Mango, Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.
 
Mbali a burudani kutoka kwa Twanga Pepeta, siku hiyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau, wakongwe wa muziki wa dansi nchini, bendi ya Mlimani Park maarufu kwa mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.
 
Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema kuwa kila kitu kimekamilika, huku akiamini kuwa mashabiki wao watapataa kitu adimu kutoka kwao.
 
Alisema kuwa nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Nyumbani ni Nyumbani, Ngumu Kumeza, Mwenda Pole, Kila Nifanyalo, Shamba la Twanga na Twanga 2013.
 
Albamu nyingine za bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001),  Chuki  Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari (2005),Password (2006),  Mtaa wa Kwanza (2007),  Mwana Dar es Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment