Pages

Pages

Sunday, June 30, 2013

Mtibwa yasimamisha kwanza usajili wao kwa ajili ya vigogo wa Simba na Yanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, amesema kwa sasa wameacha kwanza suala la usajili hadi watakapogundua kuwa timu kongwe za Simba na Yanga zimemaliza, ili kuepusha migogoro inayotokea mara kwa mara kutokana na kuchukua hata wale walioingia mkataba na timu nyingine.
Mexky Mexime, Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar
Sakata la usajili kwa klabu za Ligi Kuu limeibua msisimko wa aina yake, huku timu za Simba, Yanga na Coastal Union zikionekana kugongana vichwa kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mexime alisema kuwa mara nyingi timu za Simba na Yanga zimekuwa zikileta vurugu katika suala zima la usajili, hivyo wameamua kwanza wasubiri wao wamalize ndio wasajili, hasa kwa kuangalia mnyukano unaoendelea.
 
Alisema wao wanaamini kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka, hivyo hawawezi kuathiriwa, hasa kwa kuamua kupisha keleleza Simba na Yanga.

“Unaweza kumsajili mchezaji au kuwa na mipango naye, lakini inapotokea anawindwa na Simba au Yanga, basi huwa kwenye matatizo ya kila aina, hivyo ni bora wafanye kwanza wao.
 
“Sisi tupo imara na tunajiamini, ndio maana tuna uwezo wa kuchukua hata wale ambao wanaona si lolote na kuwapika ndani ya timu yetu, wakati wao wanasubiri wale waliotengenezwa,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Mexime, uamuzi huo uliangaliwa kwa kina na kusema kamwe hauwezi kuwaathiri kwa kutangaza kuacha kusajili hadi Simba na Yanga wamalize, ikiwa ni njia ya kuepusha mkanganyiko kwenye mpira wa miguu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment