Pages

Pages

Sunday, June 16, 2013

Taifa Stars wapeni raha Watanzania leo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU ya Taifa, Taifa Stars, leo inashuka katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumenyana na timu ya Taifa ya Ivory Coast, katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Mrisho Ngassa, mmoja wa nyota wa Stars.....
Stars inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa Morocco, huku ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 6 nyuma ya Ivory Coast yenye pointi 10, huku Morocco wakishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi tano, huku Gambia yenyewe ikibaki na pointi moja.

Mechi hiyo ni mwendelezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, huku Stars ikiwa katika kundi C, ambapo ina kila sababu ya kushinda leo dhidi ua Ivory Coast kaam inajitaji kujieka katika mazingira mazuri ya kufuzu katika fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2014, nchini Brazil.

Timu ya Taifa, Taifa Stars iliyoweka kambi yake katika Hoteli ya Tamfoma, bado ina nafasi ya kuweza kufuzu kama itashinda katika michezo yake iliyosalia na kuwapa raha Watanzania.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Meck  Sadiki, alitembelea katika kikosi cha Stara na kuwapa moyo wa kuhakikisha kuwa wanafanya vyema mbele ya Ivory Coast na kufufua matumaini ya kufuzu katika michuano hiyo.

Alitumia nafasi hiyo pia kuwapa salamu za Rais Jakaya Mrisho Kikwete, juu ya kuwafunga Ivory Coast, ambaye ndio anayeongoza kundi C, ambaye pia imewasili Tanzania ikiwa na lengo la kushinda katika uwanja wa ugenini.

“Tunataka ushindi na sio kuogopa majina ya wachezaji hawa wa Ivory Coast maana ni wenye miguu kama nyie, huku tukiamini kuwa Stars mnaweza kufanya vyema na kulitangaza Taifa katika mpira wa miguu, hivyo fanyeni bidii,” alisema Sadik.

Nahodha wa Stars, Juma Kaseja, aliwahakikishia Watanzania kuwa watacheza kufa na kupona katika kuhakikisha kuwa wanafanya vyema katika mchezo huo muhimu kwao.

“Tunatambua moyo wa uzalendo uliopo kwa Watanzania dhidi yetu, hivyo nitashirikiana na wenzangu katika kuona tunashinda katika mechi ya Ivory Coast katika uwanja wetu wa nyumbani.

“Tunajiamini kwa kiasi kikubwa kuwa tunaweza kufanya vizuri katika mchezo wetu huu, hivyo tunaomba Watanzania waje kwa wingi kushangalia kwa ajili ya kuwafunga Ivory Coast,” alisema Kaseja.

Stars inanolewa na kocha wake Kim Poulsen, huku akiwa na shauku ya kuona timu yake inafuzu katika michuano ya Kombe la Dunia, endapo itashinda katika mechi zake zilizosalia.

No comments:

Post a Comment