Pages

Pages

Sunday, June 16, 2013

Binslum aichokonoa Simba na Yanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa benchi la ufundi laa timu ya Coastal Union, ambaye pia ni mdhamini wa klabu hiyo, Nassoro Binslum, amesema klabu za Simba na Yanga zina mtaji mkubwa wa wanachama wenye nazo, ila zinashangaza pale zinapokosa maendeleo ya soka la Kimataifa.
Nassor Ahmed Binslum
Coastal imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya sita, huku ikipania kujiwekea mikakati kabambe kwa ajili ya kuiongoza timu yao, hasa kwa kuwasajili Haruna Moshi Boban na Juma Nyosso, wote kutoka katika timu ya Simba.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Bin Slum, alisema kwamba Simba na Yanga zimesheheni wanachama na wapenzi wa kila aina, wakiwapo viongozi wa serikali na wafanya biadhara wenye nazo.

Alisema kwasababu hiyo, wana kila sababu ya kujiendesha kimataifa, hasa kwa kucheza soka lenye ubora sambamba na kuwania mataji makubwa duniani ngazi ya klabu.

“Nashangaa kwanini hizi klabu hazina maendeleo wakati zina mtaji mkubwa wa wanachama na wapenzi ambao wengi wao wana nafasi kubwa, hivyo huu ni udhaifu wa aina yake.

“Nafasi waliyokuwa nayo hawa wanaoitwa wakongwe, endapo wangeipata watu kama sisi, hakika tungevuka malengo ya timu ya TP Mazembe, ambayo leo imekuwa tishio Afrika,” alisema Bin Slum.

Bin Slum ni miongoni mwa wadau wa mpira wa miguu wanaojipambanua vilivyo kuhakikisha kuwa mkoa wa Tanga unarudi kwenye chati zake kwa kuhakikisha kuwa Coastal Union inatamba ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment